"Mtaji wazo VS Mtaji Fedha "
Swala la nini kinapaswa kuwa cha
kwanza kati ya mtaji wa fedha na wazo la kibiashara limewatatiza wengi
sawa na shairi lile la Darasa la tano liliouliza "YAI AU KUKU NANI KATANGULIA?".
Uhalisia ni kwamba hata fedha yenyewe ni wazo na kimsingi kitu chochote
cha kushikika kilitokana na wazo fulani na badae wazo hilo likawekwa
katika uhalisia.
Juzi nilikuwa naongea na watu fulani nikawaambia
kwamba siku zote mtaji fedha hufuata mtaji wazo .Yapo mawazo ambayo
yanakupa mbinu za kupata fedha hivyo basi tatizo kubwa tusiseme ni
mtaji fedha lakini wengi tuna tatizo la kukosa mtaji wazo.
Ukweli
ni kwamba watu wengi hatuna mawazo .Kwa mujibu wa mwandishi wa
vitabu,mhamasishaji na mwanzilishi wa makanisa ya winners chappel Pator
David Oyedepo anasema 5% ya watu wote duniani ndio wenye mawazo, 15% ya
watu wanadhani kuwa wanawaza kumbe hawawazi na 80% ya watu wote duniani
wanakufa bila kuwaza(hii ni hatari).
Napoleon Hill aliwahi
kuuliza swali "if you get a million dollar what will you do???".
Napoleon Hill alitambua kuwa binadamu wengi wanalamika hawana fedha huku
wakiwa hawana mawazo ya nini watafanya baada ya kupata fedha .Wewe ni
shahidi umekuwa ukipata pesa mara ngapi na umezifanyia nini(unajua
mwenyewe).
Watu wengi wana fedha lakini hawana mawazo sasa kwako
wewe hii ni fursa ya kutumia mtaji wazo kupata hizi fedha ambazo hazina
kazi zimekaa tu .Shida wengi hatutaki kuumiza vichwa na kuzalisha mawazo
yenye tija (productive ideas).
Kama wewe una sh laki moja na
unahitaji kuanza biashara ya laki sita na huna fedha hiyo kwanini
usiungane na marafiki wazuri 6 ulionao wenye uwezo wa kupata laki moja
kwa mwezi mkafanya mchezo na ukapata hiyo pesa kiulaini???(umekosa
mawazo siyo mtaji).
Kuna watu hapa mjini ni madalali wa mambo
lukuki na wanapata hela sana bila kutumia hata chembe ya shillingi
.Fikiria dalali anapangisha watu watano au kumi kwa mwezi anapata sh
ngapi ?? bado dalali huyu huyu yuko kwenye viwanja, kumbi n.k .Mtu huyu
anapata pesa nyingi .Kuwa dalali siyo kwamba hujasoma acha mawazo potofu
.Dalali ni Third part anayekurahisishia kupata huduma uitakayo haraka
hata wewe unaweza kuamua kuwa dalali na ukaendelea na maisha (tumekuwa
vipofu)
Acha kabisa kulalamika kuwa huna mtaji wakati huo una
simu ya laki saba na unaweka vifurushi vya elfu moja kila siku na
kupanda bodaboda kila siku
No comments:
Post a Comment