Saturday, July 9, 2016

MUSA SAID AREJEA KUTOKA KATIKA KAMBI YA KIMATAIFA YA COPA COCA- COLA, UFARANSA

Nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari akiwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. 
Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga (kushoto) akimpokea kwa shangwe nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari (katikati) mara baada ya kuwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. Pembeni ni Pamela Lugenge (kulia) mmoja wa Afisa Masoko. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. 
Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga (kushoto) akimkabidhi taji la maua nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari mara baada ya kuwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. Pembeni ni Pamela Lugenge (kulia) mmoja wa Afisa Masoko. 

USHUHUDA VIDEO

WAZIRI, NAPE AZINDUA MASHINDANO JIJINI DAR ES SALAM LEO.

Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya magari jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akiwa amenyanyua bendera ya Taifa juu kuashiria uzinduzi wa Mashindano ya Mbio za Magari ya 2016 jijini Dar es Salaam leo .Kulia kwa Nape ni Katibu wa Balaza la Michezo Tanzania(BMT), Mohamed Kiganja. 

UTITIRI WA VIKUNDI HUIBUKA KATIKA KIPINDI CHA UCHAGUZI-DK.MWAKYEMBE.


Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati mkutano wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) juu ya utekelezaji wa agizo la kusitisha usajili bodi za wadhamini, Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RITA, Emmy Hudson (Kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Harrison Mwakyembe la kusitisha usajili wa bodi za wadhamini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome.
Sehemu ya wajumbe wa bodi wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.

RAIS MSTAAFU DK. JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA NMB SABASABA



Meneja wa banda la Benki ya NMB katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016, Josephiner Kulwa (kushoto), akimkaribisha Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete alipotembelea banda hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
Hapa Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo.
Meneja wa banda la Benki ya NMB katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016, Josephiner Kulwa (kushoto), akitoa maelezo kwa Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete (katikati), akitoka katika banda la Benki ya NMB alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016 yanayoendelea katika viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo . Kulia ni Meneja wa banda hilo, Josephiner Kulwa na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka. Maonesho hayo yatafikia tamati kesho kutwa.

ELIMU NA AFYA NI HAKI YA MAMA NA MTOTO

"Mtaji wazo VS Mtaji Fedha "
Swala la nini kinapaswa kuwa cha kwanza kati ya mtaji wa fedha na wazo la kibiashara limewatatiza wengi sawa na shairi lile la Darasa la tano liliouliza "YAI AU KUKU NANI KATANGULIA?".
Uhalisia ni kwamba hata fedha yenyewe ni wazo na kimsingi kitu chochote cha kushikika kilitokana na wazo fulani na badae wazo hilo likawekwa katika uhalisia.
Juzi nilikuwa naongea na watu fulani nikawaambia kwamba siku zote mtaji fedha hufuata mtaji wazo .Yapo mawazo ambayo yanakupa mbinu za kupata fedha hivyo basi tatizo kubwa tusiseme ni mtaji fedha lakini wengi tuna tatizo la kukosa mtaji wazo.
Ukweli ni kwamba watu wengi hatuna mawazo .Kwa mujibu wa mwandishi wa vitabu,mhamasishaji na mwanzilishi wa makanisa ya winners chappel Pator David Oyedepo anasema 5% ya watu wote duniani ndio wenye mawazo, 15% ya watu wanadhani kuwa wanawaza kumbe hawawazi na 80% ya watu wote duniani wanakufa bila kuwaza(hii ni hatari).
Napoleon Hill aliwahi kuuliza swali "if you get a million dollar what will you do???". Napoleon Hill alitambua kuwa binadamu wengi wanalamika hawana fedha huku wakiwa hawana mawazo ya nini watafanya baada ya kupata fedha .Wewe ni shahidi umekuwa ukipata pesa mara ngapi na umezifanyia nini(unajua mwenyewe).
Watu wengi wana fedha lakini hawana mawazo sasa kwako wewe hii ni fursa ya kutumia mtaji wazo kupata hizi fedha ambazo hazina kazi zimekaa tu .Shida wengi hatutaki kuumiza vichwa na kuzalisha mawazo yenye tija (productive ideas).
Kama wewe una sh laki moja na unahitaji kuanza biashara ya laki sita na huna fedha hiyo kwanini usiungane na marafiki wazuri 6 ulionao wenye uwezo wa kupata laki moja kwa mwezi mkafanya mchezo na ukapata hiyo pesa kiulaini???(umekosa mawazo siyo mtaji).
Kuna watu hapa mjini ni madalali wa mambo lukuki na wanapata hela sana bila kutumia hata chembe ya shillingi .Fikiria dalali anapangisha watu watano au kumi kwa mwezi anapata sh ngapi ?? bado dalali huyu huyu yuko kwenye viwanja, kumbi n.k .Mtu huyu anapata pesa nyingi .Kuwa dalali siyo kwamba hujasoma acha mawazo potofu .Dalali ni Third part anayekurahisishia kupata huduma uitakayo haraka hata wewe unaweza kuamua kuwa dalali na ukaendelea na maisha (tumekuwa vipofu)
Acha kabisa kulalamika kuwa huna mtaji wakati huo una simu ya laki saba na unaweka vifurushi vya elfu moja kila siku na kupanda bodaboda kila siku

INTRODUCING KIJANA JITHAMINI